Kalengo awatisha mabeki Ligi Kuu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Jul 2019
Kalengo awatisha mabeki Ligi Kuu

Mshambuliaji Yanga, Mzambia Maybin Kalengo, ametoa vitisho kwa mabeki wa timu pinzani baada ya kusema kuwa yupo Yanga kwa ajili ya kufunga mabao, hivyo hatatishika na beki yeyoye kwenye Ligi Kuu Bara na mashindano yote ambayo kikosi chake kitashiriki.

Baada ya kukaa nje kwa takriban wiki moja akiuguza majeraha ya kifundo cha mguu, jana asubuhi straika huyo alianza mazoezi mepesi.

Kalengo amejiunga na Yanga hivi karibuni akitokea Zesco FC ya Zambia, lakini tangu amejiunga na kambi ya Yanga amejikuta akikaa nje kwa takriban wiki moja kufuatia kuwa na majeraha kwenye kifundo chake cha mguu

Straika huyo ni miongoni mwa wachezaji wa Yanga ambao wanatarajiwa kutambulishwa Agosti 4, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar katika Tamasha la Siku ya Mwananchi ambapo huenda wakacheza na Rayon Sports

Kalengo alisema kwa kuwa ameanza mazoezi ana imani kubwa ya kuwepo kwenye mchezo huo

"Natamani sana siku hiyo ya tamasha la kilele cha Siku ya Mwananchi nipate nafasi ya kucheza, hivyo namuomba Mungu anijalie uzima ili niweze kuonyesha nilichonacho,"

"Mbali na hilo, mimi ni mshambuliaji, hivyo suala la kufunga kwangu sio la kuuliza, nitafunga bila ya kumhofia beki wa aina yoyote"

Kalengo alianza vizuri maisha yake kunako klabu ya Yanga kabla ya kupata majeraha hayo ya kifundo cha mguu

Hakuweza kucheza katika michezo yote mitatu ya kirafiki ambayo timu hiyo imecheza mkoani Morogoro

GPL

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
6h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
14h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
21h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’