Kiwango kinachoonyeshwa mazoezini na mlinda lango Ramadhani Kabwili kimemvutia kocha wa makipa Peter Manyika ambaye amekiri ushindani utakuwa mkubwa kati ya makipa wanne waliosajiliwa
Kabwili aliongezwa mkataba kuendelea kuitumikia Yanga ukiwa ni mpango wa muda mrefu wa mabingwa hao wa kihistoria kuendelea kumlea kipa huyo mwenye umri wa miaka 18
Manyika amesema kama Kabwili ataendeleza ubora alionao sasa, huenda akawapa wakati mgumu Farouk Shikalo na Metacha Mnata ambao wengi wanatarajia ndio watakuwa chaguo la kwanza langoni
Leo Kabwili alianza langoni kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya ATN Academy, mchezo ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 7-0
Mkenya Shikalo tayari ametua mkoani Morogoro huku Metacha akiondoka kujiunga na kambi ya Stars
Β