Mlinda lango mpya wa Yanga Farouk Shikalo tayari ametua mkoani Morogoro kuungana na wenzake kwenye kambi ya maandalizi ya msimu mpya
Mlinda lango huyo aliyesajiliwa na Yanga akitokea klabu ya Bandari Fc, leo atajumuika na wachezaji wengine wanaoendelea kujifua mkoani Morogoro
Shikalo amekamilisha idadi ya walinda lango wanne waliosajiliwa na Yanga msimu huu
Hata hivyo baada ya Metacha Mnata kujiunga na kambi ya timu ya Taifa, Mkufunzi wa makipa Peter Manyika ataendelea kubaki na makipa watatu kambini ambao ni Shikalo, Kabwili na Kindoki
ADVERTISE HERE