Yanga yajipanga upya baada ya Ratiba ya CAF

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Jul 2019
Yanga yajipanga upya baada ya Ratiba ya CAF

Yanga italazimika kufanya mabadiliko ya program zake hasa baada ya hapo jana Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) kutoa ratiba ya michezo ya awali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika

Mabingwa hao wa kihistoria watacheza na Towship Rollers katika mchezo ambao huenda ukapangwa kupigwa siku ya Jumamosi, August 10 katika uwanja wa Taifa

Hivi karibuni uongozi wa Yanga uliweka hadharani mipango yake ya kwenda kuweka kambi nje ya nchi baada ya ratiba ya ligi ya mabingwa kutolewa

Hata hivyo kutokana muda mfupi uliobaki kuelekea mchezo wa kwanza, Yanga inaweza kuendelea kujifua hapahapa Tanzania na baada ya mchezo wa kwanza ikaelekea Afrika Kusini kuweka kambi ya maandalizi ya mchezo wa pili utakaopigwa kati ya August 23-25 huko Botswana

Aidha August 04 Yanga itacheza mchezo muhimu wa kuhitimisha wiki ya Mwananchi, mchezo ambao utatumika kutambulisha kikosi pamoja na jezi za timu hiyo kuelekea msimu ujao

Hata hivyo uongozi wa timu hiyo huenda ukalazimika kutafuta timu nyingine ya kucheza nao August 04 baada ya AS Vita nao kubanwa na ratiba ya mchezo wa awali ligi ya mabingwa

Uongozi wa Yanga leo ulipanga kuzungumza na waandishi wa habari lakini Mkutano huo umeahirishwa ili kuwapa nafasi viongozi wa timu hiyo kujipanga upya baada ya mabadiliko hayo ya ratiba

Aidha kesho Jumanne Yanga ilipaswa kuwa mkoani Dodoma kumenyana na Dodoma Fc kwenye mchezo wa kirafiki, taarifa zinabainisha mchezo huo huenda ukaahirishwa

Kwa sasa kikosi cha Yanga kinaendelea kujifua mkoani Morogoro

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
32m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’