Mshambuliaji Sadney Urikhob alichelewa kuripoti kambini mkoani Morogoro kwa takribani wiki moja baada ya kukabiliwa na changamoto ya pasi ya kusafiria
Hata hivyo mshambuliaji huyo raia wa Namibia, ameonyesha kujitambua baada ya kuomba apewe muda zaidi wa kufanya mazoezi ili awe 'fit' sawa na wenzake ambao kesho Jumatatu wataingia wiki ya tatu tangu waanze kujifua mkoani humo
Juzi Sadney alipaswa kucheza katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Moro Kids lakini badala yake akaomba apewe program ya mazoezi na kocha Noel Mwandila
Kumekuwa na ushindani mkali wa namba kwenye kikosi cha Yanga hali inayowafanya wachezaji 'wajiongeze' kwa kufanya mazoezi ya ziada ili waweze kuwa imara
Juzi alipotembelea kambi mkoani Morogoro, Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla aliwasifu wachezaji wa timu hiyo akibainisha kuwa msimu ujao wapinzani wajiandae kwelikweli kukabiliana na vijana hao ambao wameonyesha kuwa na ari na ushindani mkubwa