Baada ya kucheza michezo miwili ya kirafiki mkoani Morogoro, kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuelekea mkoani Dodoma kuumana na Dodoma Fc katika mchezo mwingine wa kirafiki utakaopigwa uwanja wa Jamhuri keshokutwa Jumanne, Julai 23 2019
Mratibu wa Yanga Hafidh Saleh amesema ni muhimu kwa timu hiyo kupata michezo mingi ya kirafiki kujipima kabla ya kuanza mikiki mikiki ya ligi na michuano ya Kimataifa
"Tunahitaji kucheza michezo mingi ya kirafiki, hatuwezi kufanya mazoezi tu bila ya kujipima," amesema
"Kama hakutakuwa na mabadiliko tarehe 23 tunakwenda kucheza na Dodoma Fc"
Yanga iliyoweka kambi mkoani Morogoro, ilianza kwa kuifumua Tanzanite Fc mabao 10-1 kisha kuichapa Morogoro Kids mabao 2-0 juzi
Baada ya mchezo wa Jumanne, Yanga huenda ikacheza mchezo mwingine kabla ya kuikaili AS Vita katikay mchezo wa kilele cha wiki ya Mwananchi utakaopigwa August 04 kwenye uwanja wa Taifa