Wakati mlinda lango mpya wa Yanga Farouk Shikalo akitarajiwa kuwasili leo kujiunga na kambi ya timu hiyo mkoani Morogoro, kocha Mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera huenda akawasali siku ya Jumatano au Alhamisi ijayo, imefahamika
Taarifa za uhakika ni kwamba Shikalo atatua leo na kuelekea moja kwa moja kambini mkoani Morogoro
Shikalo ni mchezaji pekee wa kigeni ambaye mpaka sasa bado hajawasili kambini
Usajili wa Shikalo ambaye alikuwa mlinda lango wa Bandari Fc, umezungumzwa sana
Mtihani wake wa kwanza ndani ya kikosi cha Yanga ni kufikia matarajio ya mashabiki wengi ambao wamejenga imani kubwa kwake
ADVERTISE HERE