Dk Msolla awataka wachezaji watambue ukubwa wa Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Jul 2019
Dk Msolla awataka wachezaji watambue ukubwa wa Yanga

Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amewataka wachezaji wa timu hiyo wajitambue na wajisikie fahari kuchezea Yanga

Dk Msolla na baadhi ya viongozi waandamizi wa Yanga jana walishuhudia mazoezi ya timu hiyo mkoani Morogoro ukiwemo mchezo wa kirafiki dhidi ya Moro Kids

Baada ya mchezo huo, Dk Msolla alipata nafasi ya kuzungumza na wachezaji ambapo aliwataka kutimiza majukumu yao ipasavyo ili kuhakikisha timu hiyo inatimiza malengo iliyojiwekea msimu huu

Aidha Dk Msolla alisema atatafuta muda mzuri zaidi kuweza kuzungumza na wachezaji hao mmoja mmoja

"Wote mliosajiliwa Yanga mna vipaji, tunataka mtumie vipaji vyenu kuipa mafanikio timu kwenye michuano yote tutakayoshiriki," alisema

Dk Msolla pia alipata nafasi ya kuzungumza na Wanachama wa klabu ya Yanga mkoani Morogoro ambapo aliwapa jukumu la kuhakikisha kambi ya timu hiyo inakuwa ya mafanikio makubwa

Yanga imekamilisha wiki mbili tangu itue mkoani Morogoro kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu ya Tanzania Bara pamoja na michuano mingine

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’