Sawa, kocha alaumiwe lakini Yanga ina matatizo zaidi

Mchambuzi Huru By Mchambuzi Huru
β€’
24 Sep 2017
Sawa, kocha alaumiwe lakini Yanga ina matatizo zaidi
Moja ya michezo ambayo Yanga haikuwafurahisha mashabiki wake ni mchezo dhidi ya Ndanda licha kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Japo lawama nyingi zimesukumwa kwa kocha George Lwandamina ambapo kimsingi ni sahihi kwa sababu yeye ndiye 'bosi' mtoa maamuzi wa mwisho juu ya nani acheze na nani atoke, bado binafsi sikuridhishwa na juhudi zilizofanywa na mchezaji mmoja mmoja hasa kwenye safu ya ushambuliaji.

Morali ya baadhi ya wachezaji ilionekana kuwa chini sana, sijafahamu wachezaji wa Yanga wamekumbwa na nini kwani tatizo hili limekuwa likijitokeza kwenye karibu kila mchezo ukiondoa ule wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba.

Lazima ifahamike kama kuna matatizo nje ya uwanja yanaweza kuwaondoa wachezaji mchezoni.

Jana Donald Ngoma hakuwa kwenye kiwango bora kabisa, alifanya makosa mengi sana, achilia mbali kukosa mabao mepesi.

Chirwa nae hivyo hivyo. Wengi walitegemea Ajib angeendelea kubaki dimbani na Chirwa au Ngoma mmoja wapo alistahili kupumzishwa.

Chirwa anaweza akatetewa kwa kuwa alikaa nje kwa karibu miezi miwili nadhani atarejea kwenye kiwango chake anahitaji muda.

Bado upana wa kikosi cha Yanga ni changamoto pia. Labda Amissi Tambwe atakaporejea ataweza kuongeza nguvu hasa kwenye safu ya ushambuliaji.

Yanga haina wachezaji wa akiba ambao wanaweza kubadili taswira ya mchezo ukilinganisha na wapinzani wao Simba.

Wakati mwingine unaweza ukaielewa hofu ya kocha Lwandamina kwenye kufanya mabadiliko kwani anafahamu uwezo wa wachezaji wake.

Licha ya kuwa na vijana wenye vipaji nje lakini sio rahisi kwa kocha kuwaingiza mara moja kwenye kikosi cha kwanza kwani uzoefu ni muhimu pia.

Kutokana na ushindani mkubwa uliopo kwenye ligi kocha hapati nafasi ya kujaribu baadhi ya wachezaji kuwapa uzoefu.

Bahati mbaya Yanga imekuwa ikipata ushindi kwa taabu. Timu inapofunga mabao mengi mwalimu anaweza kutumia dakika kadhaa za mchezo kujaribu wachezaji.

Lakini sio rahisi timu inapoongoza kwa mfano bao moja mwalimu akatoa wachezaji wazoefu labda wawe wameumia.

Yanga inahitaji Mechi zaidi kukiamsha kikosi. Si vibaya viongozi wakatafuta mchezo japo mmoja wa kirafiki baada ya mchezo dhidi ya Mtibwa wakati ligi itakaposimama kupisha kalenda ya FIFA.

Benchi la Ufundi linapaswa kuhakikisha kikosi kinarudi kwenye makali yake mapema kabla ya mchezo wa kwanza dhidi ya Simba unaotarajiwa kupigwa mwezi ujao, Oktoba 28.

Kwa uchezaji huu wa sasa, sioni Yanga ikiifunga Simba kwa namna yoyote.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
19h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
23h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’