Wikiendi hii kocha Mwinyi Zahera atakuwa mkoani Morogoro kuungana na benchi la ufundi kukinoa kikosi cha Yanga kuelekea msimu mpya
Huu ni msimu muhimu sana kwake kwani wengi wanasubiri kwa hamu kuona aina ya timu atakayotengeneza
Msimu uliopita Yanga ilimaliza nafasi ya pili kwenye ligi, mafanikio hayo yalichukuliwa kama 'maajabu' kutokana na changamoto zilizoikabili timu hiyo
Pamoja na udogo wa kikosi chake kilichokuwa na matatizo mengi, Zahera aliweza kutengeneza timu imara ambayo kuna wakati iliwatia presha hata Simba ambao ubingwa wao unaonekana kusaidiwa na mbeleko ya TFF
Msimu huu Yanga imesajili kwa kufuata mapendekezo ya Zahera
Kwa maana nyingine, msimu huu unaoanza mwezi ujao, Zahera atakuwa na timu yake aliyoipendekeza
Hivi karibuni wakati akihojiwa nchini Misri baada ya DR Congo kutolewa kwenye michuano ya Afcon, Zahera alisema ni mchezaji mmoja tu ambaye alisajiliwa hakumpendekeza awali, Muharami Issa 'Marcelo'
Hata hivvyo alibariki usajili huo baada ya aliyekuwa beki wa kushoto Gadiel Michael kufanya 'maringo'
Zahera ana kazi kubwa tatu mbele yake ambazo anapaswa kuzifanya ili kibarua chake kiendelee kuwa salama
Kwanza ni kurudisha ubingwa wa ligi kuu Jangwani
Katika kipindi cha miaka 20, Yanga haijawahi kukaa zaidi ya misimu miwili bila ya kutwaa ubingwa
Huu umekuwa utamaduni na Zahera anafahamu bila ubingwa kurudi nyumbani, anaweza kukumbana na wakati mgumu ingawa uongozi wa Yanga umesema unafikiria kumpa muda mrefu ili ajenge timu
Lakini hili litategemea na mafanikio atakayopata mwishoni mwa msimu
Inaendelea......