Pamoja na mtihani wa kurejesha ubingwa wa ligi kuu Jangwani, jambo la pili Zahera atakuwa na mtihani wa kuhakikisha Yanga inafanya vizuri kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Mafanikio iliyopata Simba kwenye michuano hiyo msimu uliopita kwa kufika robo fainali, ni mtihani kwake
Kwani kama Yanga itatolewa kwenye hatua za awali, na kwa usajili huu uliofanyika, maswali yanaweza kuwa mengi
Jambo la tatu ambalo ni muhimu zaidi ni kupata ushindi dhidi ya Simba
Ingawa michezo ya watani wa jadi msimu mzima inaweza kuwa miwili tu, lakini michezo hii ndiyo inayoongoza kwa kufukuzisha kazi makocha
Msimu uliopita Wanayanga walifahamu hali ya timu yao na ndio maana hawakulalamika baada ya kufungwa kwenye mchezo wa pili wa ligi kuu ya Tanzania Bara
Lakini hali itakuwa tofauti msimu ujao hasa baada ya timu kuboreshwa, kufungwa na Simba ni jambo ambalo halitavumilika
Tangu mwaka 2016 mashabiki wa Yanga hawajashangilia ushindi dhidi ya Simba. Hans van Pluijm ndio kocha wa mwisho kuifunga Simba
Zahera ana kazi kurudisha umwamba wa Yanga katika michezo ya 'derby' dhidi ya Simba kwani takwimu zinaonyesha Yanga ndio timu iliyoshinda michezo mingi dhidi ya Simba
Yanga pia itashiriki michuano mingine kama kombe la FA (ASFC) ambalo bingwa wake anajihakikishia nafasi ya kucheza michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika. Pia michuano ya Sportpesa Cup na kombe la Mapinduzi
Ubingwa wa kombe la FA unaweza kuwa muhimu pia, kwani inapotokea Yanga ikakosa ubingwa wa ligi kuu, kupitia michuano hiyo itajihakikishia kucheza michuano ya Kimataifa