Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera anatarajiwa kuwasili wakati wowote baada ya kumaliza likizo
Zahera aliyekuwa nchini Misri na kikosi cha timu ya Taifa ya DR Congo, alielekea nchini Ufaransa kwa ajili ya mapumziko ya wiki moja baada ya DR Congo kutolewa kwenye michuano ya Afcon hatua ya 16 bora
Mcongomani huyo alisema anakwenda kuiona familia yake kwa siku chache kabla ya kurejea nchini kuendelea na majukumu ya kuinoa Yanga
Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema Zahera amemaliza muda wake wa mapumziko na wakati wowote atawasili na kuelekea moja kwa moja mkoani Morogoro kuungana na kambi ya Yanga
ADVERTISE HERE