Klabu ya AS Vita imethibitisha kuwa August 04 itakuwa Tanzania kucheza na mabingwa wa kihistoria Yanga kwenye mchezo wa Kimataifa wa kirafiki
AS Vita inayonolewa na Florent Ibenge kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya DR Congo, wamesema mchezo huo ni sehemu ya maandalizi yao kuelekea msimu mpya
Yanga itautumia mchezo huo kutambulisha kikosi chake cha msimu ujao
Aidha mchezo huo utawakutanisha makocha Ibenge na Mwinyi Zahera ambao wanafanya kazi pamoja katika timu ya Taifa
Zahera ni kocha msaidizi wa DR Congo
ADVERTISE HERE