Mlinda lango wa Yanga Farouq Shikalo atajiunga na timu hiyo wiki ijayo baada ya kumaliza mapumziko
Shikalo alishiriki michuano ya Afcon na kikosi cha Harambee Stars na baadae kuunganisha nchini Rwanda kushiriki michuano ya kombe la Kagame akiwa na Bandari Fc
Mchezaji huyo hakupata muda wa mapumziko kama ilivyokuwa kwa wachezaji wote walioshiriki michuano ya Afcon
"Nataka nipumzike kwa siku saba hapa nyumbani unajua sijapumzika kabisa, baada ya siku hizo nitakuwa Tanzania kujiunga na Yanga, kwani nimeshamaliza kazi Bandari, " alisema Shikalo akiwa nchini Kenya
Msimu huu Yanga itakuwa na walinda lango wanne, Shikalo akitarajiwa kuwa mlinda lango namba moja
Wengine ni Metacha Mnata, Ramadhani Kabwili na Klaus Kindoki
Kindoki huenda akaondoka wakati wa usajili wa dirisha dogo mkataba wake utakapokuwa umemalizika
Wachezaji wote tayari wameripoti kambini mkoani Morogoro isipokuwa Shikalo na mshambuliaji Sadney Urikhob ambaye ujio wake bado unasubiriwa
Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema kutokamilika kwa vibali vya kazi ni moja ya sababu zinazomchelewesha Sadney