Yanga yapiga hesabu hatua ya makundi ligi ya mabingwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Jul 2019
Yanga yapiga hesabu hatua ya makundi ligi ya mabingwa

Mwezi ujao Yanga inarejea kwenye mikiki mikiki ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika baada ya kukosa kwa msimu mmoja

Mabingwa hao wa kihistoria wanasubiri kumfahamu mpinzani wao watakaocheza nae kwenye mchezo wa hatua ya awali utakaopigwa kati ya August 09-11

CAF itafanya droo baada ya kumalizika michuano ya Afcon

Msimu huu Yanga imejiwekea malengo ya kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo mikubwa kabisa barani Afrika kwa ngazi ya vilabu

Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Yanga imecheza hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho mara mbili lakini upande wa ligi ya mabingwa, kwa mara ya mwisho Yanga ilicheza hatua hiyo mwaka 1998

Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amesema ingawa waliipata nafasi ya kushiriki michuano hiyo kwa kuchelewa, lakini wamejiwekea malengo ya kutinga hatua ya makundi

Amesema kwa usajili makini waliofanya anaamini wana nafasi kubwa ya kufanya vizuri na kufika mbali zaidi katika michuano hiyo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
10h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
14h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
15h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
15h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’