Beki Ally Mtoni 'Sonso' tayari yuko kambini mkoani Morogoro akijiunga na kikosi cha Yanga kinachoendelea na maandalizi ya msimu mpya
Sonso aliyetua Yanga akitokea klabu ya Lipulu Fc, ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa wamepewa mapumziko kutokana na ushiriki wao kwenye michuano ya Afcon
Beki huyo kisiki ameungana na mkongwe na nahodha Kelvin Yondani ambaye Sonso amemuelezea kama beki bora Tanzania na amekuwa akijifunza mambo mengi kutoka kwake
ADVERTISE HERE