Uongozi wa klabu ya Yanga unakusudia kutumia tukio la siku ya Mwananchi August 04 kuwaaga waliokuwa nyota wa timu hiyo Thabani Kamusoko na Amissi Tambwe
Tambwe na Kamusoko ni miongoni mwa wachezaji walioipa Yanga heshima kubwa ikiwemo kuisaidia kutwaa mataji matatu ya ligi kuu ya Tanzania Bara mfululizo
"Ukizungumzia wachezaji waliokuwa na mchango mkubwa kwa Yanga hutakosa kuwataja Kamusoko na Tambwe"
"Tumepanga kuwaalika siku ya Mwananchi ili mashabiki wapate nafasi ya kuwaaga na kuwashukuru kwa mchango waliotoa kwenye timu yetu," amesema Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela
Tambwe alitua Yanga mwezi Disemba mwaka 2014 akifunga jumla ya mabao 73 kwenye ligi wakati Kamusoko alisajiliwa na Yanga mwaka 2015 ambapo ujio wake ulinogesha aina ya uchezaji wa Yanga kwenye sehemu ya kiungo
Kamusoko ndiye muasisi wa mtindo wa 'kampa-kampatena'
Wachezaji hao wameruhusiwa kuondoka baada ya kutokuwa kwenye mipango ya kocha Mwinyi Zahera kwa ajili ya msimu ujao