AS Vita kipimo sahihi kwa nyota wapya - Fei Toto

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Jul 2019
AS Vita kipimo sahihi kwa nyota wapya - Fei Toto

Kiungo wa Yanga, Feisal Salum 'Fei Toto' amesema mchezo wao dhidi ya AS Vita ni kipimo tosha kwao kuonyesha ubora wa nyota wapya waliosajiliwa na kudhihilisha maandalizi waliyofanya.

Fei Toto ameungana na kikosi Morogoro leo baada ya mapumziko ya wiki mbili waliyopewa kutokana na kutoka katika majukumu ya timu ya Taifa Taifa Stars iliyokuwa ikishiriki mashindano ya AFCON, Stars haikufanikiwa kushinda mechi hata moja.

Fei Toto alisema aliposikia taarifa za kukutana na AS Vita alifurahia kwani aliamini ni mchezo ambao utaonyesha mwanga wa ubora wa kikosi chao kabla ya Ligi Kuu aijaanza huku akibainisha kuwa ndio mchezo utakaotoa taswira nani yuko fiti.

"Ni timu kubwa na bora itasaidia kwa namna moja au nyingine kutuonyesha nani ni bora zaidi ya mwenzake naamini mwalimu atatoa nafasi kwa nyota wote kucheza katika mchezo huo kwa lengo la kusuka kikosi chake bora cha ligi msimu unaokuja"

"Bado sijafanya mazoezi na nyota wapya waliosajiliwa Yanga kujua ubora wao japo kuna ninao wafahamu kama Makame ambaye nimeshacheza naye naamini muda ukifika kila mmoja atajionea ubora wa mmoja mmoja," alisema Fei Toto.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’