Mratibu wa Yanga Hafidh Saleh amesema kiungo mshambuliaji wa timu hiyo Mrisho Ngasa amepata msiba wa kufiwa na babu yake hivyo amepewa ruhusa ya kwenda kuzika mkoani Shinyanga
Ngasa amekuwepo kambini mkoani Morogoro tangu Julai 08 Yanga ilipoanza kujifua mkoani humo
Hafidh amesema wachezaji wengine wako katika hali nzuri wakiendelea na mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya siku ya Mwananchi pamoja na msimu mpya wa ligi kuu ya Tanzania Bara na Michuano ya ligi ya mabingwa
Katika hatua nyingine, Hafidh amesema mpaka kesho Jumapili wachezaji zaidi wanatarajiwa kuwasili kambini
Baadhi ya wachezaji waliokuwa nchini Misri kushiriki michuano ya Afcon 2019, walipewa mapumziko ya siku 10
Miongoni mwa wachezaji ambao hawakuripoti kambini ni pamoja na Sadney Urikhob ambaye alitarajiwa kuwasili kutoka Namibia jana na walinda lango Metacha Mnata na Farouq Shikalo
Shikalo alikuwa Rwanda na kikosi cha Bandari Fc kilichokuwa kinashiriki michuano ya kombe la Kagame
Hata hivyo timu hiyo imetolewa kwenye michuano hiyo
Shikalo atajiunga na kambi ya Yanga baada ya kumaliza majukumu ya timu hiyo
Tayari uongozi wa Yanga na Bandari Fc wamemalizana kuhusu sintofahamu ya usajili wake