Kocha mpya wa makipa Peter Manyika ametua mkoani Morogoro na kuanza kazi ya kuwanoa makipa wa Yanga
Taarifa ya Manyika kuchukua nafasi ya mkongwe Juma Pondamali ilivuja wiki iliyopita na jana Manyika alianza rasmi kazi ya kuwanoa walinzi hao wa lango
Manyika aliwahi kutamba akiwa na kikosi cha Yanga mwishoni mwa miaka ya 90 kabla ya kustaafu na kuendelea na majukumu akiwa kocha
Alikuwa kocha wa makipa wa kikosi cha timu ya Taifa ya vijana, Serengeti Boys
Atakuwa na kazi ya kuhakikisha viwango vya walinda lango wa Yanga Farouq Shikalo, Metacha Mnata, Klaus Kindoki na Ramadhani Kabwili vinakuwa kwenye ubora wakati wote
ADVERTISE HERE