Licha ya kuelezwa mkataba wake na Yanga unamalizika Septemba, uongozi wa Yanga umesema hauna kinyongo kwe aliyekuwa beki wake Gadiel Michael kuitumikia Simba
Gadiel ametambulishwa leo kunako klabu ya Simba baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili
Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema walichukua hatua mapema kumuondoa kikosini beki huyo wa timu ya Taifa hivyo wamemtakia kila la kheri huko alikoelekea
Gadiel alikuwa 'akiuhadaa' uongozi wa Yanga kuhusu kusaini mkataba mpya kabla ya viongozi kumshitukia na kusajili mbadala wake Muharami Issa 'Marcelo'
Gadiel ameungana na aliyekuwa nahodha wa Yanga Ibrahim Ajib ambaye naye alijiunga na Simba
Kocha Mkuu wa Yanga amesema timu yake imesajili wachezaji bora hivyo hadhani kama kuondoka kwa wachezaji hao kutawaathiri msimu ujao