Ligi kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2019/20 inatarajiwa kuanza August 23 ambapo Yanga itaanza kampeni ya kusaka ubingwa kwa kuumana na Ruvu Shooting August 28
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura amesema mchezo wa kwanza wa watani wa jadi kati ya Simba dhidi ya Yanga utapigwa Januari 04 2020 Yanga ikianzia ugenini
Aidha, mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Simba dhidi ya Azam Fc utapigwa August 17 kwenye uwanja ambao utatangazwa baadae
Wambura amesema upangaji wa ratiba msimu huu umezingatia kalenda za michuano ya CAF na FIFA
ADVERTISE HERE