Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuondoka jijini Dar es Salaam kesho Jumatatu kuelekea mkoani Morogoro kuanza kambi ya maandalizi ya msimu mpya
Nyota waliosajiliwa na timu hiyo walianza kuwasili tangu juzi tayari kwa kambi hiyo itakayokuwa Bigwa nje kidogo ya mji wa Morogoro
Awali kulikuwa na taarifa kwamba Yanga ingeweka kambi nje ya nchi lakini ufinyu wa muda imetajwa kuwa sababu ya kujichimbia Morogoro
Julai 27 ni siku kubwa kwa Wanayanga ambapo timu yao itatambulisha kikosi kwa kucheza mchezo wa kirafiki uwanja wa Taifa
Kocha Noel Mwandila ana kazi ya kuhakikisha Yanga iliyosheheni sura nyingi ngeni, inakuwa tayari kwa mchezo huo
Agosti 09-11 Yanga itashuka dimbani kuanza kampeni ya michuano ya ligi ya mabingwa hatua ya awali
Ratiba ya michezo ya awali itapangwa baada ya kumalizika michuano ya Afcon inayoendelea nchini Misri