Klabu ya Yanga inatarajiwa kuanza kujifua rasmi kesho Jumapili, Julai 07 ikianza maandalizi ya msimu mpya pamoja na kilele cha siku ya Mwananchi Julai 27
Nyota wa kigeni wa timu hiyo walianza kuwasili jana ambapo leo nyota zaidi watawasili kuungana na wachezaji wazawa
Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Dismas Ten amesema mazoezi yataanza kesho lakini program rasmi itaanza siku ya Jumatatu
Mazoezi yatakuwa chini ya kocha Msaidizi Noel Mwandila
Taarifa za awali zimebainisha kuwa Yanga huenda ikaelekea mkoani Morogoro kuweka kambi yake
ADVERTISE HERE