Kikosi cha Yanga leo kimeendelea na mazoezi kwenye dimba la Uhuru kujiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Ndanda utakaopigwa keshokutwa Jumamosi.
Ukiondoa Beno Kakolanya na Amissi Tambwe wachezaji wengine wote walishiriki kwenye mazoezi hayo yaliyosimamiwa na kocha Mkuu George Lwandamina akisaidiana na Shedrack Nsajigwa.

Baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Majimaji mchezo uliopita, kikosi cha Yanga kimedhamiria kuondoka na alama zote tatu kwenye mchezo dhidi ya Ndanda FC.
Kikosi cha Ndanda nacho kimeweka kambi mkoani Morogoro kujiandaa na mchezo huo.

ADVERTISE HERE