Msuva akumbuka kiroba cha mchele alichopewa na Ali Yanga

Admin By Admin
•
23 Jun 2017
Msuva akumbuka kiroba cha mchele alichopewa na Ali Yanga
Winga wa Yanga SC, Simon Msuva amesema ameumizwa na kifo cha aliyekuwa shabiki mkubwa wa timu hiyo, Ally Mohammed ‘Ally Yanga’ aliyefariki dunia juzi Dodoma.

“Kifo cha Ally Yanga kimeniuma sana, maana alikuwa ni zaidi ya shabiki kwangu, kwa sababu alikuwa ananiambia vitu vingi sana hasa katika soka letu la Tanzania.

Kikubwa ambacho sitakuja kukisahau ni siku ambayo alinikabidhi kiroba cha mchele Uwanja wa Taifa baada ya kumaliza mechi, kwa kweli sina mengi ya kuzungumzia juu ya Ally Yanga, ila imeniuma sana kumpoteza shabiki huyu mzalendo," amesema Msuva.

Ally Yanga alifariki baada ya ajali ya gari akiwa kwenye msafara wa mbio za Mwenge kabla ya kupata ajali hiyo barabara ya Wiyenzele kuelekea Chipogoro na kufariki hapo hapo.

Ally aliyezaliwa mkoani Shinyanga Machi 1, mwaka 1984 katika familia ya watoto sita, kabla ya umauti wake inafahamika alikuwa anaishi Yombo Vituka, Dar es Salaam.

Lakini amezikwa Shinyanga baada ya kuagwa jana Dodoma.

Aliibukia Ubungo miaka ya nyuma kidogo ambako alikuwa anafanya shughuli ya kusajili laini za simu za mkononi katika vibanda vilivyokuwa pembeni ya kituo kikuu cha mabasi ya mikoani, Ubungo Terminal.

Na alianza kuonekana Uwanja wa Taifa pamoja na kikundi cha mashabiki wa Yanga cha Ubungo Terminal, ambako ndipo lilipokuwa tawi lake.

Lakini tangu baada ya uchaguzi Mkuu Novemba 2015, Ally Yanga ameadimika viwanja vya soka kutokana na kujikita zaidi kwenye shughuli za Chama cha Mapinduzi CCM.

Ally hakuwa shabiki wa Yanga tu, enzi za uhai wake alikuwa akizishabiki pia timu za taifa, kuanzia za vijana na wakubwa za wanawake na wanaume.

Alikuwa maarufu Afrika Mashariki kutokana na kwenda kuishabikia Taifa Stars kwenye mechi za Kombe la CECAFA Challenge nchi za Kenya na Uganda.

Lakini pia amewahi kusafiri hadi nje ya Afrika Mashariki akiwa na Taifa Stars kwenye mechi za kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika na Kombe ka Dunia.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →