Yanga yapania kutinga fainali SportPesa

Admin By Admin
•
8 Jun 2017
Yanga yapania kutinga fainali SportPesa
Baada ya kuitoa Tusker FC, ya Kenya kwenye michuano ya Sport Pesa Super Cup, kikosi cha Yanga Alhamisi kitakuwa na kibarua kingine cha kuwania kutinga fainali wakati itakapo wakabili wababe wengine kutoka Kenya AFC Leopard.

Yanga ambao ndiyo timu pekee ya Tanzania iliyobaki kwenye michuano hiyo baada ya klabu za Simba, Singida United na Jang’ombe Boyz kutolewa kwenye mechi zao za awali ilifika hatua hiyo kwa kuitoa Tusker wakati AFC Leopards waliitoa Singida United.

Timu zote zililazimika kufika katika changamoto ya mikwaju ya panalti baada ya kutoka nguvu sawa katika muda wa kawaida.
Yanga ambao ndiyo wenyeji pekee waliosalia kwenye michuano hiyo wanalazimika kupambana ili kutinga fainali na kutwaa ubingwa huo ili kufuta aibu ya timu nyingine zilizotolewa na kucheza na Everton Julai 13.

Kocha Juma Mwambisi ambaye ndiyo anaiongoza Yanga kwenye michuano hiyo, amesema utakuwa mchezo mgumu kwasababu AFC Leopards ni timu nzuri na wanakikosi chao kamili tofauti na wao.

“Tumejipanga kuhakikisha tunacheza vizuri na kupata ushindi lengo ni kucheza fainali na kutwaa ubingwa hasa tukitambua kuwa ndiyo timu pekee ya Tanzania katika michuano hii,”amesema Mwambusi.

Kocha huyo amesema kikosi chake cha kesho hakitakuwa na mabadiliko makubwa kwani asilimia kubwa ya wachezaji wake itakuwa ni walewale vijana na anaimani nao ya kumaliza mchezo mapema kabla ya kufikia kwenye matuta.

Amesema katika safu ya ushambuliaji atamtegemea zaidi mshambuliaji Obrey Chirwa, ambaye na Said Salum ambaye aliingia kipindi cha pili kwenye mchezo dhidi ya Tusker huku safu yake ya ulinzi ikibaki vilevile kama ilivyokuwa kwenye mchezo wa awali.

Kwaupande wake kocha Dennis Kitambi wa AFC Leopard amesema wamejipanga kucheza kwa kiwango cha juu zaidi ya ilivyokua kwenye mchezo wa kwanza kwasababu wanahitaji kucheza fainali.

Kitambi raia wa Tanzania amesema anawaheshimu Yanga kuwa ni timu kubwa na wana nacheza mbele ya mashabiki wao lakini wamejiimarisha kuhakikisha wanapambana na kushinda mchezo huo.

“Nimchezo mgumu siyo kwetu bali hata Yanga, kitu kizuri nimewaona wanavyocheza na nikazi yangu kuchagua mfumo wa kutumia ili kupata ushindi,”amesema Kitambi.

Mshambuliaji Paoul Kiongera anatarajia kuongoza mashambulizi ya AFC Leopards na anatarajiwa kupata wakati mgumu mbele ya walinzi wa Yanga akina Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Pato Ngonyani.

Nusufainali nyingine hapo kesho itazikutanisha timu zote za Kenya mabingwa wa zamani Gor Mahia na Nakuru All Stars mchezo ambao unatarajiwa kuwa mgumu na ushindani mkali.

Gor Mahia itaingia kwenye mchezo huo huku ikimtegemea mshambuliaji wake mkongwe Medie Kagere, wakati Nakuru wenyewe watakuwa wakimuangalia Kamau Daniel na Maina Geofrey ambao wameonyesha ni moto wa kuotea mbali pindi wanapopata nafasi.

Kwa hisani ya GOAL
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
9h ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
14h ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
18h ago
READ MORE →
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
19h ago
READ MORE →
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
19h ago
READ MORE →
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
20h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE →
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE →
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE →
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE →