Beki Gadiel Michael alirejea jana na kikosi cha timu ya Taifa akitokea Misri ambako alishiriki michuano ya Afcon 2019
Hatma ya beki huyo itafahamika leo baada ya uongozi wa Yanga kumtaka asaini mkataba au aseme kama hana mpango wa kuendelea kucheza Jangwani
Gadiel amekuwa akikwepa kusaini mkataba aliopewa kabla hajatimkia Misri na timu ya Taifa ikielezwa beki huyo anasikilizia ofa ya moja ya timu kutoka nje ya nchi
Hata hivyo Yanga inatarajiwa kuanza mazoezi ya maandalizi ya msimu mpya wiki ijayo, wametaka kukamilisha usajili mapema
Aidha Julai 10 ndio siku ya mwisho kuwasilisha majina ya wachezaji waliosajiliwa kwa ajili ya michuano ya ligi ya mabingwa bila faini
ADVERTISE HERE