Tshishimbi apania kurudi kivingine msimu ujao

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Jul 2019
Tshishimbi apania kurudi kivingine msimu ujao

Kiungo wa Yanga Mkongomani Papy Tshishimbi amesema ametumia likizo yake kurudisha makali yake baada ya kumaliza msimu uliopita vibaya.

Tshishimbi anatarajia kutua nchini kesho tayari kwaajili ya kuingia kambini kujiandaa na mchezo wao wa kimataifa wa kirafiki maalum kwaajili ya kutambulisha wachezaji wapya unaotarajiwa kufanyika Agosti 3 Mwaka huu.

Tshishimbi alisema yupo fiti na amejiandaa kuhakikisha anacheza michezo yote ya ligi endapo atapewa nafasi na mwalimu huku akiomba Mungu kumuepusha na majeraha ya mara kwa mara kama ilivyokuwa msimu uliopita

"Unajua ni ajabu sana mimi kucheza nusu dakika katika mchezo mimi nilivyokuwa nacheza Mbabane Swallows ya Swaziland, nakumbuka nilicheza dakika zote tisini michezo yote ya ligi na kucheza mashindano ya klabu bingwa hadi hatua ya makundi tuliyofika nilikosa mchezo mmoja tu nilikuwa na matatizo ya kifamilia."

"Huwezi kuamini siku nacheza na Simba mchezo wangu wa kwanza kabisa nimetua nilifanya mazoezi siku tatu tu na kiwango changu kilikuwa bora, lakini tangu hapo sielewi nilikumbwa na nini nikawa natolewa bila kumaliza dakika zote jambo ambalo lilikuwa kama suprise kwangu,"

"Sitaki hilo lijirudie tena nimetumia mapumziko vizuri kwa kufanya mazoezi mara mbili kwa siku asubuhi na jioni yote ni kuhakikisha najiweka fiti ili kulipa muda ambao sitajatumika mzunguko wa pili msimu ulioisha kuwaaminisha viongozi na mashabiki kuwa viongozi hawajakosea kuniongeza mkataba," alisema Tshishimbi.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
19h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
23h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’