Wachezaji wapya wa kigeni Yanga wanatarajiwa kuanza kuwasili leo tayari kwa kuanza maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu ya Tanzania Bara pamoja na michuano ya Kimataifa
Yanga imepanga kuanza mazoezi Julai 07, ambapo kikosi cha timu hiyo kinatarajiwa kuelekea mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki
Mratibu wa Yanga Hafidh Saleh amesema nyota anayetangulia kuwasili leo ni mshambuliaji Maybin Kalengo aliyesajiliwa kutoka klabu ya Zesco United ya Zambia
Nyota wengine watawasili Ijumaa na Jumamosi kuungana na wachezaji wazawa
Yanga imesajili wachezaji nane wa kigeni ambao ni Farouq Shikalo, Mustapha Suleyman, Lamine Moro, Issa Bigirimana, Patrick Sibomana, Juma Balinya, Sadney Urikhob na Maybin Kalengo
ADVERTISE HERE