Aliyekuwa nahodha wa Yanga Ibrahim Ajib ametambulishwa rasmi kunako klabu ya Simba baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili
Ajib ameondoka Yanga baada ya kuifanya vyema kazi yake msimu uliopita
Katika miaka yake miwili aliyocheza Yanga, Ajib amefunga mabao 13 na kutoa pasi za mabao zaidi ya 20
Msimu ulipita aliibuka nyota wa pasi za mabao, akitoa pasi 15 huku akifunga mabao sita
Tunamshukuru kwa huduma yake, tunamtakia kila la kheri huko alikochagua kwenda kuendeleza maisha yake ya soka...!
ADVERTISE HERE