Wakati anaanza kuinoa Yanga, kocha Mwinyi Zahera alisaini mkataba wa muda mfupi kutokana na mazingira yaliyokuwepo wakati huo
Hata hivyo licha ya changamoto ambazo amekumbana nazo Yanga, Mcongomani huyo aliendelea na majukumu yake jambo lililowashangaza wengi
Mwishoni mwa mwaka jana Zahera alipata ofa ya kujiunga na Buildcon Fc ya Zambia iliyokuwa imemtengea mshahara wa Tsh Milioni 34 lakini alikataa
Yanga imepiga hatua chini ya Zahera kwani ukiachana na kazi yake aliyoifanya uwanjani, Mcongomani huyo ndiye aliyebuni mpango wa kuwashirikisha mashabiki waichangie timu yao
Alifungua akaunti maalum ya kukusanya fedha, akaunti ambayo ilikuwa na watia saini watatu ili kuhakikisha fedha za Wanayanga zinakuwa salama ili baadae zitumike katika lengo lililokusudiwa la kukiboresha kikosi
Leo hii Yanga imefanya usajili wa kishindo na kila mmoja anajivunia hatua hii ambayo mwanzoni wapo walioamini isingefanikiwa
Kutokana na haya, sio ajabu kwa uongozi wa Yanga kumuandalia Zahera mkataba wa muda mrefu
Kocha huyo Msaidizi wa timu ya Taifa ya DR Congo anatarajiwa kusaini mkataba mpya atakaporejea kutoka Misri