Beki mpya wa Yanga Ally Mtoni 'Sonso' ameeleza furaha yake baada ya kukamilisha usajili wake wa kutua Yanga nchini Misri
Sonso alisaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Yanga akiwa Misri na kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kinachoshiriki fainali za Afcon 2019
Amesema anafurahishwa na uchezaji wa beki kisiki Kevin Yondani na kwa mda mrefu alikuwa akitamani kucheza timu moja na mkongwe huyo
"Yondani ni beki mzuri sana hakuna asiyefahamu hilo na mimi nilikuwa natamani siku moja nicheze naye timu moja kwani kwa uwezo wake mzuri alionao, tukicheza wote hakuna mtu wa kutusumbua kabisa," amesema
Sonso amesema anaamini uwepo wa Yondani kwenye kikosi cha Yanga msimu ujao, pamoja na ujio wa nyota wapya akiwemo yeye, utazidi kuimarisha safu ya ulinzi ya Yanga
Mbali na Sonso, Yanga pia imewasajili walinzi wa kati Lamine Moro kutoka Ghana, Mustapha Suleyman kutoka Burundi na Ally Ally kutoka klabu ya KMC