Jengo la Jangwani kupunguza gharama za uendeshaji Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Jul 2019
Jengo la Jangwani kupunguza gharama za uendeshaji Yanga

Uongozi wa Yanga uko kwenye mchakato wa kulifanyia ukarabati jengo lake lililopo Jangwani hasa kukarabati vyumba vya wachezaji

Hivi karibuni Yanga ilitangaza kuwaalika wadau mbalimbali wa klabu hiyo kujitolea kukarabati chumba/vyumba ili kuiwezesha timu hiyo kuanza kulitumia

Aidha zoezi hilo linakwenda sambamba na ukarabati wa uwanja wa Kaunda ambao utatumika kwa ajili ya mazoezi

Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amesema zoezi hilo likikamilika Yanga itapunguza gharama kubwa za kuweka wachezaji Hoteli pamoja na gharama za kukodi viwanja vya mazoezi

"Jengo hili tulilonalo ndio kitega uchumi kikubwa cha klabu. Ukiacha mambo ya mishahara, gharama kubwa za timu ni mambo ya Hoteli na kukodi viwanja vya mazoezi" amesema Dk Msolla

"Tumekuwa tukilipa mamilioni ya shilingi kulipia Hotel na kukodi viwanja. Lakini tukitengeneza hapa fedha hizo zitatusaidia katika masuala mengine ya kuiendesha timu"

cut

Jengo la Jangwani lina vyumba 28 kwa ajili ya wachezaji. Hata hivyo kwa miaka mingo vyumba hivyo vimeachwa bila kutumika huku klabu ikitumia gharama kubwa kuweka kambi Hotelini

Mpango huo ukikamilika utakuwa na manufaa makubwa kwa Yanga

Aidha uongozi wa Yanga umekusudia kutumia eneo la ekari saba walilopewa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda huko Kigamboni kujenga uwanja Mkubwa wa klabu, viwanja viwili vya mazoezi na Shule ya kukuzia vipaji

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’