Baada ya kukamilisha usajili wa beki wa Lipuli Fc Ally Mtoni 'Sonso', safu ya ulinzi ya Yanga ina wachezaji saba wanaocheza kati
Mabeki wapya wa kati ni Lamine Moro, Mustafa Suleyman, Ally Ally na Ally Mtoni wakati Kelvin Yondani, Andrew Vicent na Abdallah Shaibu waliitumikia Yanga msimu uliopita
Yondani na Dante bado wana mkataba na Yanga hivyo kuna uwezekano mdogo kwa Ninja ambaye mkataba wake umemalizika kuendelea kubaki Yanga
Nafasi pekee iliyopo ni kumuongezea mkataba kisha kumtoa kwa mkopo jambo ambalo wachezaji wengi ambao mikataba yao imemalizika huwa hawapendelei
ADVERTISE HERE