Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera yuko Misri na kikosi cha DR Congo kushiriki michuano ya Afcon 2019 inayoendelea nchini humo
Zahera tayari ametuma program yake ya mazoezi kuelekea msimu mpya ambapo uongozi wa Yanga uko kwenye mchakato wa kukamilisha mahitaji ya kambi
Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amesema wameipokea program hiyo mapema wiki hii na sasa wanashughulikia mahitaji ya kambi
Yanga inatarajiwa kwenda kuweka kambi nje ya nchi kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya na michuano ya ligi ya mabingwa
Aidha Julai 27 Yanga itacheza mchezo wa Kimataifa wa kirafiki ikiwa ni siku ya kilele cha wiki ya Mwananchi
Mchezo huo ambao utapigwa uwanja wa Taifa, utaambatana na matukio ya utambulisho wa jezi pamoja na kikosi cha Yanga
Dk Msolla amethibitisha kuwa kambi ya Yanga itasimamiwa na Zahera mwenyewe anayetarajiwa kurejea mapema baada ya DR Congo kuondoshwa kwenye hatua ya makundi michuano ya Afcon 2019