Kiungo wa Yanga Mcongomani Papi Tshishimbi yuko mapumziko kwao DR Congo baada ya kumalizika msimu wa ligi kuu ya Tanzania Bara
Akiwa na rafiki zake maeneo mbalimbali, uzi ya Yanga umeonekana kutamalaki
Hilo linathibitisha kuwa uzi wa timu ya Wananchi umevuka mipaka mpaka huko DR Congo wanaufurahia..!
Tshishimbi ataendelea kuitumikia Yanga kwa misimu mingine miwili akiwa amesaini mkataba mpya kabla ya kurejea kwao
Ukiondoa majeruhi yaliyomsumbua msimu uliopita, Tshishimbi amekuwa na mafanikio kunako klabu ya Yanga, na bila shaka ataendelea kun'gara kwenye kikosi kipya cha mabingwa hao wa kihistoria ambacho kitakuwa na mafundi wengi wa mpira
ADVERTISE HERE