Aliyekuwa kiungo wa Singida United Kenny Ally ambaye alitarajiwa kujiunga na Yanga ikiwa ni ahadi ya Dk Mwigulu Nchemba, amejiunga na KMC
Taarifa za uhakika zinabainisha kuwa Kenny amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia KMC
Juni 15 kulikuwa na Harambee ya kuichangia Yanga iliyofahamika kama Kubwa Kuliko ambapo Dk Mwigulu, Rais wa Singida United ambaye ni mwanachama wa Yanga, aliahidi kukamilisha usajili wa mchezaji mmoja mzawa ikiwa ni sehemu ya mchango wake kwa timu hiyo
Kenny Ally ndiye mchezaji aliyekuwa akitajwa kwenye mpango huo wa Dk Nchemba
Kenny atajiunga rasmi na KMC baada ya mkataba wake kumalizika Juni 30 2019
ADVERTISE HERE