Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Emmanuel Amunike amekiri kutofurahishwa na kadi za mara kwa mara anazopewa kiungo Feisal Salum 'Fei Toto'
Juzi Fei Toto alipata nafasi ya kucheza mchezo dhidi ya Senegal michuano ya Afcon 2019 inayoendelea huko Misri
Hata hivyo presha ya mchezo huo ilipelekea Fei Toto apewe kadi ya njano mapema tu na akafanyiwa mabadiliko kabla ya mapumziko kutokana na kuwepo uwezekano wa kupewa kadi ya pili ya njano
Amunike amesema kadi za njano zina athari kwenye mashindano hayo
"Nimekuwa nikimfuatilia Fei Toto, amekuwa na kadi nyingi za njano hata kwenye klabu yake," amesema
"Muhimu namuelekeza ajiepushe na matukio yasiyo ya lazima kuyafanya, nafanya hivyo kwa wachezaji wote"
"Kwa mashindano haya hatupaswi kuwa na wachezaji wengi wenye kadi, kwani zinaweza kutuathiri mbeleni"
Kwenye ligi iliyomalizika, Fei Toto alikosa michezo mitatu kutokana na kutumikia adhabu za njano