Julai 27 2019 itakuwa siku ya kipekee kwa Wanajangwani kwani siku hiyo kutakuwa na tukio kubwa la kuhitimisha wiki ya Mwananchi litakalofanyika uwanja wa Taifa
Kuanzia saa sita kamili mchana, Burudani mbalimbali zitarindima uwanja wa Taifa kisha kufuatiwa na mchezo wa kirafiki wa kukata na shoka ambao utatumika kukitambulisha kikosi cha Yanga cha msimu wa 2019/20
Baada ya kushiriki kikamilifu kwenye kampeni mbalimbali za kuichangia Yanga, siku hiyo itakuwa ya furaha kwa Wanajangwani kwani watakuwa na nafasi ya kushudia matunda ya kazi yao
Tukio hili sio la kushuhudia kwenye TV, kila Mwanajangwani anapaswa kuwemo dimbani ili kuwadhihirishia wale wenye mashaka kuhusu mashabiki wa Yanga kuujaza uwanja wa Taifa
ADVERTISE HERE