Tambwe bado hayuko tayari kurejea dimbani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Sep 2017
Tambwe bado hayuko tayari kurejea dimbani
Mashabiki wa klabu ya Yanga huenda wakalazimika kusubiri kwa muda mrefu zaidi kumuona mshambuliaji wao Amissi Tambwe ambaye maumivu ya goti yamemuweka nje.

Taarifa iliyotolewa na Daktari wa Yanga, Dk Edward Bavu imebainisha kuwa Tambwe bado anaendelea na program maalum ya mazoezi ya viungo Hospitalini.

Mara ya mwisho Tambwe kuichezea Yanga ilikuwa kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Jamhuri wakati wa maandalizi kuelekea msimu mpya wa VPL.

Katika mchezo huo alicheza kwa dakika 35 tu na baadae kushindwa kucheza kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii baada ya kupata maumivu hayo siku moja kabla ya mchezo huo.

Hii si mara ya kwanza kwa Tambwe kupata madhira hayo. Msimu uliopita alikaa nje kwa zaidi ya wiki sita akisumbuliwa na matatizo hayo hayo ya goti.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
19h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
23h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’