Wakati anasajiliwa Yanga kutoka Coastal Union miaka mitatu iliyopita, winga Juma Mahadhi aliayaanza maisha yake Jangwani na 'moto mkubwa'
Mchezo aliocheza ambao unakumbukwa zaidi na wengi ni ule wa ligi ya mabingwa dhidi ya TP Mazembe ambao ulipigwa uwanja wa Taifa
Kwenye mchezo huo Mahadhi aliupiga 'mpira mwingi' mpaka kuwafanya Wanayanga waamini wamempata Msuva mpya
Hata hivyo winga huyo mwenye kasi alishindwa kuendeleza makali yake ambapo masuala binafsi na majeraha ya mara kwa mara yalimfanya aporomoke kiwango
Msimu uliopita hakucheza kabisa akiuguza majeraha ya goti aliyopata kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger
Amemaliza mkataba kunako klabu ya Yanga na inaelezwa ni miongoni mwa wachezaji ambao hawatapewa mikataba mipya
Kutokana na umri wake bado kuwa mdogo, Mahadhi ana nafasi ya kurejesha makali yake katika timu mpya itakayomsajili
Β