Jana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli alifika nyumbani kwa Mkurugenzi wa Utawala wa Kampuni ya SportPesa Abbas Tarimba kumpa pole baada ya kufiwa na watoto wake wawili wa kiume
Tarimba aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Yanga, katika kipindi cha miezi mitatu amepoteza watoto wawili kutokana na ugonjwa wa Dengue
Hivi karibuni Tarimba aliishauri Serikali kutilia mkazo udhibiti wa ugonjwa huo ambao umezidi kushika kasi jijini Dar es salaam
Katika watoto wake waliofariki, mmoja alikuwa rubani na mwingine Mhandisi wa Ndege



ADVERTISE HERE