Kindoki anaweza kutolewa kwa mkopo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Jun 2019
Kindoki anaweza kutolewa kwa mkopo

Uongozi wa Yanga uko kwenye mchakato wa kukamilisha usajili wa mlinda lango wa Bandari Fc Farouq Shikalo ambaye ni pendekezo la kocha Mwinyi Zahera

Ujio wa Shikalo utaifanya Yanga iwe na walinda lango wawili wa kigeni

Kuna taarifa kwamba ujio huo wa Shikalo utapelekea Kindoki atolewe kwa mkopo, klabu ya Singida United ikitajwa

Aidha Yanga pia inadaiwa kuwa imemsajili aliyekuwa kipa wa Azam Fc Metacha Mnata aliyeitumikia kwa mkopo Mbao FC

Licha ya mashabiki wengi kupinga uwepo wa Kindoki kwenye kikosi cha Yanga, mchezaji huyo bado ana mkataba wa mwaka mmoja

Njia pekee ya kuachana nae ni kuvunja mkataba wake kwa kumlipa fedha zilizoainishwa katika makubaliano ya mkataba au kumtoa kwa mkopo

Kindoki alisajiliwa na Yanga kuchukua nafasi ya Youthe Rostand ambaye mkataba wake ulivunjwa

Kama Yanga itavunja mkataba wa Kindoki atakuwa mlinda lango wa pili kuvunjiwa mkataba katika kipindi cha mwaka mmoja

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
35m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’