Wiki hii uongozi wa Yanga unatarajiwa kukamilisha usajili ambapo Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla ameahidi wataweka hadharani majina ya wachezaji ambao hawataendelea kuitumikia Yanga msimu ujao
Mchakato wa kuwapa mikataba mipya baadhi ya wachezaji unaendelea ambapo mpaka sasa Papi Tshishimbi, Gadiel Michael na Raphael Daudi wanatajwa kuwa tayari wameshasaini mikataba mipya
Yanga ilikuwa na wachezaji 19 ambao mikataba yao imemalizika, ukimuondoa Ajib ambaye anaondoka nyota hawa baadhi yao wanasubiri kujua hatma yao wiki hii
1. Ramadhani Kabwili
2. Juma Abdul
3. Haji Mwinyi
4. Abdallah Shaibu
5. Pato Ngonyani
6. Said Juma
7. Matheo Anthony
8. Mrisho Ngasa
9. Thabani Kamusoko
10. Pius Buswita
11. Juma Mahadhi
12. Baruani Akilimali
13. Amissi Tambwe
14. Haruna Moshi
15. Deus Kaseke
Kati ya hawa yupi Mwana Jangwani unadhani anastahili kuendelea kubaki timu ya Wananchi?