Zahera afurahia usajili Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Jun 2019
Zahera afurahia usajili Yanga

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ameupongeza uongozi wa timu hiyo kwa kufanikiwa kukamilisha usajili wa wachezaji wote aliowahitaji

Hivi karibuni Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla alisema timu hiyo imekamilisha usajili wa wachezaji wote wa kigeni waliopendekezwa na Zahera

Kwa sasa wanakamilisha usajili wa wachezaji wazawa, zoezi ambalo litafikia tamati mwishoni mwa wiki hii

"Nimefurahi wamesajili wale wachezaji wote ambao nilitaka. Msimu ujao tutakuwa na timu nzuri sana," amesema Zahera ambaye juzi kikosi chake cha DR Congo kilikubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Uganda kwenye mchezo wa kwanza wa Afcon

Mcongoman huyo amesema atarejea mara moja kujiunga na kikosi cha Yanga baada ya michuano ya Afcon kumalizika

Yanga inatarajiwa kuingia kambini Julai 07 ambapo Noel Mwandila ataanza kukinoa kikosi cha timu hiyo ambacho hakitajumuisha wachezaji wanaoshiriki Afcon

Julai 27 Yanga itahitimisha wiki ya Mwananchi kwa kucheza mchezo wa kirafiki uwanja wa Taifa

Mabingwa hao wa kihistoria wataanza kampeni ya kusaka nafasi ya kutinga hatua ya makundi michuano ligi ya mabingwa barani Afrika mwanzoni mwa mwezi wa nane

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
35m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’