Baada ya kusubiri kwa miaka 39, Stars leo inarejea uwanjani katika fainali za michuano ya Afcon 2019 itakapoikabili Senegal katika mchezo utakaopigwa uwanja wa 30 June
Watanzania tuna kila sababu ya kuiunga mkono timu yetu kwenye mchezo wa leo
Kwani baada ya kuwa mashabiki wa timu nyingine kwa miaka mingi, leo tutakuwa na nafasi ya kuishangilia timu yetu
Stars imefanya maandalizi ya kutosha na bila shaka iko tayari kwa ajili ya mchezo huo
Michezo miwili ya kirafiki waliyocheza dhidi ya Misri na Zimbabwe kabla ya michuano hiyo, ilidhihirisha uimara wa kikosi cha Amunike
Matokeo ya ushindi au hata sare kwa Stars yataongeza kujiamini kwa kikosi na lolote linaweza kutokea katika michezo mingine itakayofuata
Kila la kheri Stars, kila la kheri Tanzania..