Uongozi wa Yanga umesema wiki ijayo utaweka hadharani majina ya wachezaji ambao hawatakuwemo kwenye kikosi cha timu hiyo msimu ujao
Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amesema watawapa taarifa wachezaji hao mapema ili wasake sehemu nyingine ya kuendeleza maisha yao ya soka
Dirisha la usajili lilifunguliwa Juni 15 na litafungwa Julai 31 2019
Hata hivyo kwa Yanga inapaswa kuwa imekamilisha usajili ifikapo Juni 30 kutokana na ushiriki wake wa michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao
Dirisha la usajili la CAF litafungwa Julai mosi 2019
"Wiki ijayo tutatangaza majina ya wachezaji wote ambao hatutakuwa nao tena katika msimu ujao wa Ligi Kuu ili waanze taratibu za kutafuta maisha mengine kabla dirisha la usajili halijafungwa," amesema Dk Msolla
Hata hivyo kwa upande wa wachezaji wa kigeni Dk Msolla amebainisha kuwa ni wachezaji wawili tu ambao walikuwa nao msimu uliopita ambao watabaki
Wachezaji hao ni Klaus Kindoki na Papi Tshishimbi
Ibrahim Ajib ni mchezaji mwingine ambaye tayari uongozi wa timu hiyo umempa mkono wa 'kwa heri' akisubiri kujiunga na Simba mkataba wake utakapomalizika
Mpaka sasa Yanga imekamilisha usajili wa nyota tisa, ambapo saba ni wa kigeni na wawili ni wazawa
Timu hiyo inatarajiwa kuweka hadharani usajili wake wiki ijayo