Endelezeni eneo lenu lisipotosha nitawaongeza - Makonda

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Jun 2019
Endelezeni eneo lenu lisipotosha nitawaongeza - Makonda

Klabu ya Yanga imekabidhiwa eneo lenye ekari saba na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ukiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa wakati wa hafla ya uchangiaji ya Kubwa Kuliko.

Akikabidhi eneo hilo, lililoko kigamboni kisarawe 2, Makonda amesema eneo hilo ni Mali ya Wananchi, hivyo hata kama itatokea Yanga kuwa kampuni lakini eneo litabaki kuwa Mali ya klabu na Wanayanga.

"Naikabidhi bodi ya wadhamini, maana yake ni kwamba hili ni eneo la Wanayanga, ningeweza kukabidhi Wakurugenzi lakini wao wanaweza kufanya ujanja, ukashangaa eka mbili zimemegwa zimebaki tano," alisema Makonda.

Makonda aliwataka viongozi na Wanayanga kuanzia kujenga eneo hilo Mara moja na kuwapiku wapinzani wao Simba ambao muda mrefu tangu wapate eneo hawajafanya kinachokusudiwa.

Aidha Makonda ameitaka Yanga kujenga kwanza eneo walilopewa kisha waombe lingine kama hilo halitatosha badala ya kuomba kuongezewa eneo kabla walilonalo hawajalitumia.

Awali, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela, kwa niaba ya Wanayanga alimshukuru Makonda kwa kutoa eneo hilo kwa klabu ya Yanga na kuahidi kulitumia kwa kulingana na makusudio.

Hafla ya makabidhiano ya eneo hilo ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo wanachama na mashabiki wa Yanga

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
46m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’