Msimu uliomalizika Feisal Salum 'Fei Toto' alitumika zaidi nafasi ya kiungo mkabaji ambapo changamoto kubwa iliyokuwa ikimkabili ni kwenye ulinzi pale timu inapokuwa inashambuliwa
Baada ya Tshishimbi kuporomoka kiwango, kocha Mwinyi Zahera alilazimika kumbadilisha majukumu na kumfanya an'gare zaidi akiwa anacheza nyuma ya mshambuliaji
Tshishimbi aliweza kuifungia Yanga mabao manne
Yanga imesajili 'mkata umeme' halisi Abdulaziz Makame 'Bui' aliyetokea mafunzo ya Zanzibar
Hii ina maana, Fei Toto anaweza kusogezwa mbele zaidi na kuinufaisha Yanga kutokana na uwezo wake mkubwa wa kutawala dimba
Safu ya kiungo kwa sasa imekamilika kwa kiasi kikubwa kutokana na uwepo wa Tshishimbi pamoja na 'mapacha watatu', Mohammed Issa 'Banka', Fei Toto na Bui ambao wamekuwa wakicheza pamoja timu ya Taifa
Bado Yanga haijaweka hadharani orodha ya wachezaji wa zamani ambao wataendelea kuitumikia timu hiyo, lakini kiungo Raphael Daudi 'Lothi' anaweza kuendelea kuwemo kikosi cha Yanga msimu ujao
Aidha mazungumzo kuhusu kumuongezea mkataba mkongwe Thabani Kamusoko yako mezani hasa baada ya kiungo huyo kuonyesha uwezo mkubwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Zimbabwe akiwa miongoni mwa wachezaji wa kikosi kitakachoshiriki michuano ya Afcon inayoanza kesho huko Misri kwa Zimbabwe kuwakabili wenyeji
Kwa Yanga ilivyosajili, wengi wanatamani ligi ingeanza hata kesho waanze kupata burudani kutoka kwa mafundi hao wa mpira waliosajiliwa